Header Ads

JE, SAMATA AKAUKOSA MCHEZO WA KESHO WA TAIFA STARS VS BOTSWANA, SABABU HII HAPA




Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Jana August 31, 2017 hakuweza kumaliza hadi mwisho mazoezi pamoja na wachezaji wengine wa timu ya taifa wanaojiandaa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana.

Wakati mazoezi yanaelekea ukingoni, Samatta aliumia eneo la kisigino cha mguu wa kushoto na kulazimika kutoka nje ya uwanja kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi tulizungumza na daktari wa timu Gilbert Kigadya ili kujua Samatta anasumbuliwa na nini na kama atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Botswana.

“Tatizo lake dogo tu, ameugonga mguu chini wakati anarudisha baada ya ku-serve mpira kwa hiyo wakati anarudisha mguu chini akaugonga kwa hiyo ni maumivu madogo. nina uhakika hadi kesho atakuwa vizuri,” Kigadya.

Stars itacheza dhidi ya Botswana Jumamosi September 2, 2017 mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.

No comments

Powered by Blogger.