Header Ads

Zaidi watu 250 wameuawa kwenye maporomoko ya ardhi Sierra Leone


A picture of the mudslide
Image captionMaporomoko ya ardhi yafukia watu wengi Sierra Leone
Idadi ya watu waliouwa kwnye maporomoko ya ardhi nchini Sierra Leone haujulikani baada ya idaia tofauti kutolewa.
Shirika la habari la AP linasema kuwa takriban watu 250 wameuawa.
Eneo moja la milima liliporomoka mapema leo Jumatatu kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi kufukiwa kwa mjibu wa mwandishi wa habari wa BBC Umaru Fofana
Makamu wa rais nchini Sierra Leone Victor Bockarie Foh, alisema kuwa kuna uwezekano kuwa mamia ya watu wameuawa akiongeza kwa idadi ya watu waliouawa huenda ikaongezeka
Mwandishi wa habari aliye eneo hilo anasema kuwa watu wemgi walipatwa wakiwa bado wamelala wakati maporomoko yalitokea
Mafuriko yamekuwa makubwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMafuriko yamekuwa makubwa
"Mke wangu amekufa, watoto wangu wote wamekufa, Leo asubuhi niliongea na watoto wangu kabla ya kuenda kazini. Mmoja wao hata alinipa soksi nilizovaa." alisema mwathiriwa mmoja.
"Tulikuwa ndani, tukaskjia udongo ukikaribia, tukajaribu kukimbia, nilijaribu kumchukua mtoto wangu, lakini udongo ulikuja kwa haraka sana . Alifukiwa akiwa hai. Sijamuona mume wangu. Mtot wangu alikuwa na umri wa wiki saba." alisema muathiriwa mwingine.
Mafuriko yamekuwa makubwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMafuriko yamekuwa makubwa
Maafisa wanasema kuwa ni mapema sana kutoa idadi kamili ya watu waliouawa
Watu wamesambaza picha za uharibifu uliotokea kwenye mtandao wa twitter ya za mafuriko ndani nanje ya mji wa Free town.
Sierra Leone
Image captionSierra Leone


No comments

Powered by Blogger.