Header Ads

PICHA 2: Coutinho alivyoondoka mazoezini baada ya kuachwa katika kikosi cha game ya UEFA


Bado headlines zinazidi kuchukua nafasi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwezi huu barani Ulaya, staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea Liverpool Philippe Coutinho leo amerudi tena kwenye headlines.
Coutinho leo ameachwa katika list ya wachezaji wa Liverpool watakaosafiri kuelekea katika mchezo wa kwanza wa play off wa Champions League play dhidi ya Hoffenheim utakaochezwa kesho Jumanne ya August 15 katika uwanja wa Wirsol Rhein.
Hapa Coutinho akiondoka mazoezini akiwa ndani ya gari yake.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemuacha Coutinho katika safari ya kwenda Ujerumani kutokana na kuwa majeruhi, maamuzi ambayo baadhi ya watu wameyatafsiri kama tayari ameanza kumtoa katika hesabu zake kutokana na mchezaji huyo kuomba auzwe kwenda FC Barcelona ya Hispania.
Baada ya Neymar kujiunga na PSG ya Ufaransa kwa rekodi ya dunia ya pound milioni 199, Barcelona wanasaka saini ya Coutinho licha ya ofa yao ya pound milioni 90 ya awali kukataliwa na Liverpool.

No comments

Powered by Blogger.