Header Ads

UMESIKIA HII NDANDA DAY LITAKALOFANYIKA KESHO?




Ndanda FC inatarajiwa kufanya tamasha lao kubwa la Ndanda Day litakalofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliokuwepo Chamazi, Mbagala jijini Dar Salaam, kesho. 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo iingie udhamini   wa mwaka mmoja na Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye WhiteSands, Mbezi Beach Dar, Mkurugenzi wa Masoko wa Ndanda, Peter Simon alisema, siku hiyo wamepanga kucheza mchezo wa kirafiki majira ya saa kumi kamili jioni dhidi ya Ruvu Shooting. 

Simon alisema, siku hiyo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki wa bongo fleva ambao ni Jay Mo,  Juma Nature na Amini.

"Uongozi wa Ndanda tumepanga kutamburisha wachezaji wetu wapya ambao tumewasajili na benchi letu jipya la ufundi hiyo kesho. 

"Tumepanga tamasha letu la Ndanda Day iwe tofauti kwa maana la kuwa kubwa na kuvutia kwa mashabiki wetu wa Ndanda waishio Temeke na Mbagala na tumechagua kufanyia huko kwa sababu wengi wa Ndanda wapo maeneo hayo. 


"Hiyo kesho kabla ya shuguli asubuhi tutanya shughuli za kijamii kwa kwenda Hospitali ya Temeke wodi ya wazazi huku sherehe ikianza asubuhi saa nne, "alisema Simon.

No comments

Powered by Blogger.