Header Ads

SIMBA IMEIKUMBUSHIA YANGA ZILE GOLI 5 BAADA YA KUIADHIBU GULIONI FC, MAVUGO KATIKA UBORA WAKE.

Klabu ya soka ya Simba yenye maskani yake pale Mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam, leo imeshuka dimbani kucheza pambano la kirafiki dhidi ya timu ya Gulioni katika uwanja Amaan Zanzibar na kuibuka na ushindi mnono wa magoli 5 - 0.

Simba ambayo ipo katika mawindo dhidi ya mtani wake wa jadi Yanga ya Dar es salaam pia katika mchezo wa ngao ya jamii unataraji kupugwa Agosti 23, 2017 Jumatano pale uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam, umewatumia ujumbe mahasimu wake hao ambao waliwahi pia kuwafunga goli 5 - 0.

Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu hiyo Mrundi Laudit Mavugo leo ameibuka nyota wa ,mchezo huo kwa kuifungia timu yake magoli mawili dakika ya 16 goli la kwanza na dakika ya 39 goli la tatu. huku Shiza Kichuya katika ubora wake aliipatia timu hiyo goli la pili katika dakika 36, Juma Liuzio dakika ya 40 na Mohamed Ibrahim dakika 66 ya mchezo.


Mwalimu wa kikosi hicho Mcameroon Joseph Omog anayesaidiwa na Mganda Jackson Mayanja aliwaanzima kipa Aishi Manula, mabeki wa kati Salim Mbonde na Nahodha Methosi Mwanjali, huku pembeni ni Erasto Nyoni na Ally Shomari, viungo James Kotei, Haruna Niyonzima, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya na washambuliaji Laudit Mavugo na Juma Liuzio.

Na Shaaban Maulidi













No comments

Powered by Blogger.