Header Ads

SHAIRI: USITOE MIMBA



Shukuru wako muumba, vizuri ame kuumba
Usichana kakuremba, amekupa na mchumba
Kakunyima Na Ugumba, waweza kubeba Mimba
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Kakupa na Sura nzuri,kakupa na jina zuri
Kakupa na umbo zuri, kakupa na afya nzuri
Kakupa na dini nzuri, kakupa na hali nzuri
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Siku ulipo balehe, kwako ikawa sherehe
Kukua jua starehe, kuchi Kuchi Na Hotehe
Wala hukusamehe, ukadharau mashehe
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Kama Hukutaka ndoa, ni kwa nini ulivua
Penzi ukampatia, kwa raha nazo hisia
Tena Utamu kolea, hadi mimba kaingia
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Mama alikukataza, hiyo michezo kucheza
Kisha akakakufunza, jinsi ya kujitunza
Kiburi kimekuponza, kidoleni sasa funza
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Ukawajua shababy, mara Mume mara Hubby
Mara Sweet mara baby, mara Sam mara shebby
Mara Chande mara Phabby, ukahisi wewe Rubby
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Ukajifanya wajua, mapenzi ukayavaa
Mahaba ukayatoa, Guest mpaka Baa
Ukawa kiruka njia, leo tumbo mekujaa
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Mimba yako ni jawabu, wala sione aibu
Tena Mimba si ajabu, kutoa siyo kutubu
Itunze yako thawabu, wala sione adhabu
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Wala sije tapatapa, kutoa kisha kutupa
Riziki Mungu kukupa, itunze mithili chupa
Mungu atakuchapa, na motoni kukutupa
Dada Usitoe Mimba, mtunze Atakutunza

Ukitoa umeua, dhambi zaidi zinaa
Mlee atakulea, mwanaume kikataa
Wewe sikate tamaa, mimba sije kuitoa

Dada Sitoe Mimba, mtunze Atakutunza

No comments

Powered by Blogger.