Header Ads

GHARAMA YA SALAMU NI IPI?


Assalam alleykum, shikamoo baba, habari za asubuhi mama, u hali gani swahiba, mambo vipi rafiki, mwidiwe see. Hizi zote ni alama za salamu nasi tu kutegemeana na mtu muktadha n ahata pengine rika ndivyio vinavyozaa hizi alama za salamu.

Hata hivyo uwepo wa salamu salamu hizi haumaanishi zikae tu kama baiskeli chakavu iliyotundikwa darini yaani haina kazi labda atokee mnunua vyuma chakavu ndipo ajitose kuinunua. Kumbe basi hata salamu hizi zina umuhimu wake.

Sasa leo mwanagenzi mwenzangu wa wa Kisiwa cha Kiswahili naomba tuketi jamvini angalau tupate nasaha chache kuhusu salamu. Salamu haina gharama kama utaishi nayo lakini salamu ionagharimu kama hutoibeba salamu katika kifua chako.

Siku moja alitoka mwana wa kiume kutoka uga mmoja kuelekea uga mwingine. Alipita katikati ya msitu mnene msitu uliojaa simba ajabu lakini ni bora kungekuwa na simba. Lakini msitu ule ulijaa majoka makubwa ya kutisha kumeza kila ainba ya kiumbe mbele yake.

Basi mwana yule wa kiume aliyejinasibu kuwa jasiri tena jasiri asiye mithili aliweza kukatiza ndani ya msitu ule huku akiitafuta njia ya kumpeleka kwenye kijito ili avuke ng’ambo ya pili kwenda kutafuta kile alichodai kuwa ni dawa ya kumponya mamaye.

Basi kabla hajafika katika kile kijito alikutana na bibi kizee mmoja. Akampita bila hata kujali kwa kuwa mwili wa kikongwe kile kilikuwa kimepukutika kwa kukosa nyama. Mifupa na misuli iliyotuna kana kwamba hakuwa anakula. Aaah akampita akaenda zake.

Alivyofika mbele kidogo tu akaanza kusikia sauti za ajabu mara akatokea simba mkubwa. Mwenye macho makali macho ya rangi nyekundu. Akaanza kumkimbiza huku akitioa ngurumo kali mwana yule wa kiume akatimua mbio na kujikuta mdomoni mwa joka likammeza.

Watu walimsubiri siku na siku, majuma na majuma, miezi na miezi, miaka na mika, miongo na miongo lakini hakutokea. Hdi ynuru ya matumaini kwa wanakiji wenzake ikapotea huku mama yake akizidi kudhoofu kwa maradhi.

 Kutokana na ukimya huo, ndipo binti wa makamu binti ambaye hajavunja hata ungo, akajitosa kwenda kitafuta dawa ya mamaye. Si hilo tu lililomsukuma kwenda mwituni la hasha. Kilichomsukuma kwenda kumsaka ndugu yake wa kiume aliyepotelea tumbo la mwitu.

Basi naye aliianza safari bila ya kujua aendako. Ilimchukua majuma mawili akawa tayari amemezwa ndani yam situ ule. Punde si punde akakutana na bibi kizee kikiwa kimeshika bakora pamoja na kibuyu chenye maji kadhalika na pakacha lenye chakula.

Shikamoo bibi, alimsalimu kwa adabu na upole wa hali ya juu, marhaba yule bibi akaitikia. Kishga wakaketi chini na kuanza kuteta jambo/ Kwanza yule bibi alimpatia binti yule maji na chakula ale na kunywa  ili apate nguvu kisha akamnpatia asali ili ilwe kama tiba kwake.

Baada ya mazungumzo ya muda kadhaa bibi yule alimnuelekeza mahali ilipo dawa ya kumponya mamaye, kisha akamweleza namna ya kuvuka mto kuichukua dawa yake.Akampatia na mshale wa kumchoma nyoka aliyemmeza kaka yake.

Basi mwana yule wa kike akawa amepata dawa ya kumponya mamaye, pamoja na kumkomboa kaka yake. Na hii ni kutokana na salamu na adabu aliyoionyesha kwa bibi kizee yule ambaye kakaye alimpita bila salamu na kijikuta akiangamaia.

Sasa mwanagenzi mwenzangu nadhani kutokana na kisa hicho utakuwa umejifunza mengi juu ya umuhimu wa salamu. Kwa kuwa ubongo wako umekomaaunaweza kupembua mbivu na ,mbichi  nakuachia kazi ya kujua ni kwa vipi salamu haina gharama na kwa vipi salamu ina gharama.
Alamsiki….

Shaaban Maulidi

……………………………………………………………………………………………………..

No comments

Powered by Blogger.