Header Ads

RC PAUL MAKONDA ASHUSHA NEEMA TBC.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo ametoa msaada wa Gari aina ya Noah, Pikipiki Tatu, Computer Tano na Camera Mbili za kisasa kwa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ili kuongeza nguvu katika kuwafikia Wananchi.

Mbali na Vifaa hivyo vya kisasa pia Makonda amefanikiwa kumpata mfadhili atakaepaka Rangi Jengo lote la TBC kuanzia siku ya kesho ili liwe na mwonekano wa kisasa.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo MAKONDA amesema lengo ni kuwawezesha Wananchi ambao hawana uwezo wa kuita vyombo vya habari na kueleza matatizo yao waweze kufikiwa.

Makonda ametoa msaada huo baada ya kufika Ofisi za TBC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa ikiwemo Usafiri, Camera na Computer ambapo kwa sasa Gari na Pikipiki hizo zitawawezesha Waandishi kufika kwenye matukio kwa uharaka huku Compute zikimuwezesha  Wahariri kutekeleza majukumu yao.

Vifaa hivyo vitatumika kuongeza nguvu kwenye kipindi cha Hadubini ambacho kimekuwa kikisaidia Wananchi wanyonge kupaza sauti zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBC  Bi. MARTHA SWAI amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwapatia msaada huo kuku Zaitun Mkwama ambae ni mtayarishaji wa kipindi cha Hadubini akieleza kuwa vifaa hivyo vitawaongezea ufanisi katika kazi yao.

No comments

Powered by Blogger.