MESSI, RONALDO NA BUFFON WAINGIA FAINALI MWANASOKA BORA ULAYA
Barcelona icon Lionel Messi is also in contention for the award, which he won in 2011 and 2015 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
NYOTA
watatu, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Gianluigi Buffon wameingia
kwenye orodha fupi ya mwisho ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka
wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
UEFA
imepunguza majina kutoka 10 hadi matatu leo, huku kinda wa Monaco,
Kylian Mbappe na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Zlatan
Ibrahimovic wakiwa miongoni mwa waliokatwa.
Orodha
hiyo fupi imeteuliwa na jopo la makocha 80 wa klabu zilizoshiriki hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Europa League msimu wa 2016-2017,
pamoja na Waandishi wa Habari za Michezo 55 walioteuliwa na Kundi la
Waandishi wa Habari za Michezo Ulaya.
Ronaldo
aliisaidia Real Madrid kutwaa taji la pili mfululizo la Ligi ya
Mabingwa na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake 12.
Kipa
Buffon aliiongoza Juventus kutwaa taji la sita mfululizo la Serie A, la
tatu mfululizo la Kombe la Italia na kushika nafasi ya pili kwenye Ligi
ya Mabingwa.
Anakuwa
kipa wa pili tu kuingia tatau bora tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo msimu
wa 2010–2011, baada ya Manuel Neuer msimu wa 2013-2014.
Messi
alitwaa taji la Kombe la Mfalme maarufu kama Copa del Rey akiwa na
Barcelona na akawa mfungaji bora wa La Liga kwa mabao yake 37 msimu
uliopita.
Messi na Ronaldo wote wameshinda tuzo hiyo mara mbili, huku Mreno akiwa mshindi wa mwaka jana.
Mshambuliaji
wa VfL Wolfsburg, Pernille Harder, kiungo wa Olympique Lyon, Dzsenifer
Marozsan na winga wa Barcelona, Lieke Martens wameingia kwenye tatu bora
ya tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Mwaka Ulaya.
No comments