Header Ads

CHELSEA YAFUFUKA UGENINI KWA KUICHAPA TOTTENHAM HOSPURS, HUKU ALONSO AKING"AA.






Klabu ya soka ya Chelsea kutokea jiji la London Uingereza leo imeibua matumaini ya kutetea taji laubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kwa kuichapa Tottenham Hotspurs kwa magoli 2 - 1. Nyota ya mchezo huo iling'aa kwa Marcus Alonso aliyeifungia Chelsea magoli yote mawili katika dakika ya 24 na 88, huku Mbelgiji Mitchy Batshuayi akijifunga na kufanya mchezo umalizike kwa magili 2 -1.

Chelsea inayonolewa na Kocha Mtaliano Antonio Conte ilipoteza michezo miwli iliyopita ikiwa ule wa ngao ya jamii kwa kukubali kichapo kutoka kwa washika mitutu wa London Arsenal kwa changamoto ya Mikwaju ya penati, huku katika mchezo wa ufunguzi ikajikuta ikiadhibiwa kwenye uwanjja wake wa nyumbani magoli 3 - 2 dhidi ya Burnley.

No automatic alt text available.
Ikumbukwe ya kuwa Chelsea inawakosa nyota wake Eden Hazard, Pedro Rodriguez, Gary Cahil na wengine kwa sababu tofauti tofauti wengine wakiwa majeruhi wengine wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu.

No comments

Powered by Blogger.