Header Ads

BREKING NEWS: WANACHAMA WA SIMBA WAMEBARIKI MFUMO WA MABADILIKO.

Image may contain: one or more people and text











Siku ya leo Jumapili tarehe 20 Agosti 2017, imeingia katika rekodi mpya za soka nchini Tanzania baada ya wanachama wa klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam wamekubaliana kwa pamoja mabadiliko ya mfumo wauendeshwaji wa kalbu hiyo na sasa kuingia katika mfumo wa hisa.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Juliaus Nyerere wanachama hao walikuwa na kazi ya kubadiriki mabadaliko hayo ambayo vuguvugu lake limeanza takribani mwaka mmoja umepita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram msemaji wa klabu hiyo Haji Manara ameandika ameneno yafuatayo "wanachama wamebariki na kupitisha rasmi mfumo wa mabadiliko kwa kura nyingi za kishindo THISN IS SIMBA".

Hatua hiyo inakuwa kama mlango wa mfanyabiashara  na bilionea kijana barana Afrika Mohamed Dewj 'MO" kuwekeza hisa zake kwani kwa muda mrwefu amekuwa akihitaji suala hilo. Sasa tusibiri truone je, "MO" atapewa timu?

No comments

Powered by Blogger.