Header Ads

WATOTO WALIONUSURIKA KATIKA AJALI YA BASI LA SHULE YA LUCKY VICENT WAMEWASILI LEO.



 Siku ya Mei 26 2017 imeingia katika kumbukumbuza majonzi na simanzi kwa watanzania baada ya kutokea kwa ajali ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent kupata ajali. Tukio hilo lilisababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva wa gari hilo.

Wanafunzi 3 Sadia, Wilson na Doreen walionusulika katika ajali hiyo walipelekwa nchini Marekani kwa ajili ya kupata matibabu, na leo Ijumaa Agosti 18, watoto hao wamerejea nchini na kupokewa na wananchi na viongozi wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa KIlimanjaro Mh. Anna Mghwira katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Pia ilifanyika ibada maalumu ya shukrani na kuwaombea wenzao waliofariki.

No comments

Powered by Blogger.