Header Ads

WANAWAKE WA KIISLAMU KUVULIWA HIJAB WANAPOKWENDA KUPATA MATIBABU HUKO TANGA

24
Serikali mkoani Tanga imeahidi kuyafanyia uchuguzi madai kwamba akinamama wa Kiisalm wanalazimishwa kuvua nikab(NINJA) wanapokwenda kupata huduma katika hospital ya rufaa ya mkoa wa tanga Bombo hata baada ya kukaguliwa na walinzi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa katika hafla ya ufungaji wa kambi ya macho katika kituo cha afya cha Shifaa jijini hapa.

Amesema serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na taasisi za kidini katika kuleta maendeleo na ustawi wa jamii na kwamba madai hayo hayawezi kuachwa bila kupatiwa ufumbuzi ilikuepusha migogoro ya kidini.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Sheikh Salim Barhyani amesema taasisi ya Asaar inaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika uchumi wa viwanda kwa kuwekeza katika sekta ya afya na elimu.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema halmashauri atashirikiana na taasisi hiyo katika kutatua changamoto zinazoikabili.

Taasisi ya ansaari kwa kushirikiana na shirika la Al Basra la Saud Arabia wameendesha kambi ya aina hiyo mwak 1998, 2001, 2009 na 2015 ambapo jumla ya wagonjwa 12,162 wamechunguzwa, 3800 wamepatiwa miwani na 603 kufanyiwa upasuaji .

No comments

Powered by Blogger.