REAL MADRID YAIGARAGAZA BARCELONA NYUMBANI KWAO NOU CAMP FAINALI SUPER CUP.
Usiku wa August 13 2017 mchezo wa kwanza wa Spain Super Cup kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelonaulichezwa katika uwanja wa Nou Camp katika jiji la Barcelona, Real Madrid walikuwa ugenini katika mchezo huo uliyomalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa magoli 3-1.
Goli la kwanza la Real Madrid lilipatikana baada ya beki wa Barcelona Pique kujifunga dakika ya 50 lakini Lionel Messi akasawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 77, Cristiano Ronaldo aliyeingia dakika ya 57 akitokea benchi alifunga goli la pili dakika ya 80 na dakika ya 83 akaoneshwa kadi nyekundu kwa kujiangusha.
Licha ya Real Madrid kuwa pungufu dhidi ya FC Barcelona walifanikiwa kupata goli la tatu dakika ya 90 kupitia kwa Asensio, baada ya game hiyo FC Barcelona watahitaji ushindi wa kuanzia magoli 3-0 ili wawe Mabingwa wa Super Cup katika mchezo wa marudiano Bernabeu August 17.

No comments