Header Ads

Moto wa Bundesliga kuanza kuwaka leo, Rb Leizpg au Borussia Dortmund nani ataweza kumsimamisha Bayern Munich? By Kicki_19 - August 18, 2017



Xabi Alonso na Phillip Lahm walikuwa moja ya nguzo za mafanikio katika klabu ya Bayern Munich lakini msimu huu Bayern wanaingia bila wazoefu hao wawili ambao wametundika daluga.
Lakini bado Bayern wana matumaini kuchukua ubingwa kwa mara ya 6 mfululizo huku maingizo mapya haswa la James Rodriguez na Corentin Tolliso yakiwapa matumaini ya kutetea ubingwa wao na leo watakuwa dimbani kufungua ligi dhidi ya Bayern Leverkusen.
Msimu huu Borussia Dortmund wanaweza kuwa wapinzani wakubwa wa Bayern tofauti na ule uliopita ambapo klabu ya Rb Leizpg ndio walionekana kuitishia Bayern na kumaliza katika nafasi ya pili.
Lakini Dortmund wanaweza kuwa vizuri kama watafanikiwa kuwabakisha Osmane Dembele na Pierre Aubemayang ambao wako kwenye tishio la kuihama klabu hiyo katika dirisha hili la usajili na kocha wao mpya Peter Bosz anategemewa kuwa mhimili mpya BvB.
Rb Leizpg wamefanikiwa sana katika dirisha hili la usajili kubakisha nyota wao wakubwa Emil Forsberg na Naby Keita aliyekuwa akiwinda sana na Liverpool na hii inatoa tumaini kwa mashabiki wao.

Lakini Rb Leizpg watakuwa na Champions League hii inaweza kuwafanya wachoke na kiwatokee kilichowatokea klabu ya Leicester City msimu uliopita ambapo wingi wa michuano uliwafanya wapwaye sana.

Maingizo mapya ndani ya Rb Leizpg akiwemo mshambuliaji toka PSG Kevin Augustin na Bruma aliyesajiliwa toka Galatasaray inaweza kwa kiasi fulani kuipa nguvu Leizpg katika msimu huu wa ligi.

Bayern Leverkusen wamepoteza wachezaji wawili muhimu Javier Hernandez Chicharito aliyekwenda West Ham na Calhanoglu aliyetimkia Ac Milan ni pigo kwao lakini kocha moya Heiko Herlich anatarajiwa kutoa mbinu mpya kuibeba Leverkusen.

Hoffeinman bado hawana uhakika wa kufudhu Champions League na wasipofudhu watabaki Europa League msimu ujao wakiungana na Hertha Berlin pamoja na Cologne na hii itazifanya timu hizo kuwa na michuano ya ziada inayoweza kuwapa mzigo wa ziada katika ligi.

Stuttgart na Hannover wamepanda ligi msimu huu  lakini Stuttgart sio wageni sana kwenye ligi kwani mwaka 2015/2016 ndio walishuka daraja na mwaka huu wamerudi, kimbembe kipo kwa Hannover ambao tayari wameanza kutabiriwa kushuka daraja.

No comments

Powered by Blogger.