Header Ads

MLANDEGE WAITOA KAPA SIMBA ZENJI, SARE 0-0 AMAAN


TIMU ya Simba SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku wa leo.
Mlandege ambayo ilifungwa 2-0 na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC Jumapili usiku, leo ilikuwa mwiba kwa washindi wa taji la Azam Sports Federation Cup.
Kocha Mcameroon, Joseph Omog leo alifanya mabadiliko kidog
o kikosini mwake akiwaanzisha viungo Jonas Mkude, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na mshambuliaji Laudit Mavugo badala ya James Kotei, Emmanuel Okwi na John Bocco.
Mabadiliko hayo hakika hayakuwa na tija, kwani Simba SC ilishindwa kucheza katika ubora wake wa kwenye mechi zilizopita ikishinda 1-0 zote dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Omog kipindi cha pili, lakini hakuwatumia kabisa Okwi na Bocco kuashiria amewapumzisha kwa ajili ya mchezo ujao Jumatano dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga kuwania Ngao ya Jamii.

Simba SC imeweka kambi kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Na watani wao wa jadi, Yanga nao wapo kisiwani Pemba kwa malengo hayo hayo.
Kikosi cha Mlandege kilikuwa; Masoud Kombo, Adam Hamad, Amir William, Abubakar Mwadini, Abubakar Omar, Hassan Ramadhani, Edwin Charles, Nicholaus Frank, Shaaban Amir, Jaffar Rajab na Mohammed Abdallah.

Simba SC; Aishi Manula, Ally Shomary, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Mbonde, Method Mwanjali, Jonas Mkude/James Kotei dk76, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk84, Mohammed Ibrahim, Laudit Mavugo/Juma Luizio dk62, Haruna Niyonzima na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Jamal Mnyate dk68. 

No comments

Powered by Blogger.