Header Ads

Mahakama yawaachia huru wafuasi 13 wa CUF, Polisi ikawakamata tena…


Jeshi la Polisi na Maofisa Magereza leo August 15, 2017 lililazimika kutumia nguvu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuwadhibiti wafuasi na wanachama 13 wa Chama cha Wananchi CUF walioachiwa huru.
Wafuasi na wanachama hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa chini ya kifungu cha 225 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.
Hatua ya Polisi na Magereza kuwadhibiti wafuasi hao inatokana na kifungu hicho cha sheria kuruhu upande wa mashtaka kuwakamata tena washtakiwa pale wanapoona inafaa ambapo haikujulikana ni washtakiwa wangapi waliokamatwa kwa sababu wengi wamekimbia.

No comments

Powered by Blogger.