ILE SEMINA YA WANACHAMA WA SIMBA, INAFANYIKA KESHO NA UTARATIBU MZIMA HUU HAPA
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
15-8-2017
TAARIFA KWA UMMA
___________
Klabu ya Simba kesho inatarajiwa kufanya Semina kubwa ya Wanachama wote wa klabu hiyo.
Semina
hiyo inalenga kujenga uelewa mpana zaid juu ya muundo mpya wa klabu,
uliotokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao,na
kusajiliwa na Msajili wa Vilabu nchini.
Maandalizi
yote ya Semina hiyo yamekamilika,na itafanyika kesho tarehe
16-8-2017,Jumatano Saa Nane na Nusu mchana(8.30) na itafanyikia kwenye
ukumbi wa Mikumi uliopo kwenye eneo la maonyesho ya kimataifa ya
biashara ya Sabasaba (PTA) kurasini hapa jijini Dar es salaam.
Tunawaomba
wanachama wote popote walipo waje kwa wingi hapo kesho, huku klabu
ikiwaomba viongozi wa Simba Wilaya ya Temeke waandae utaratibu mzuri wa
kuwapokea wageni.
IMETOLEWA NA....
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
No comments