Header Ads

TUTAMSHUGHULIKIA MANGE KIMAMBI: IGP SIRRO.

 
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP) Simoni Nyakoro Sirro amesema kuwa Jeshi la polisi linatambua makosa yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi kuwa ni makosa ya kimtandao na pia Jeshi hilo linashughulikiwa suala hilo.

IGP Sirro amesema hayo jana  alipokuwa mjini Iringa kwenye ziara ambapo alisema kuwa jeshi la polisi linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ambaye amekuwa mkosoaji wa mambo mbalimbali na kutoa machapisho ambayo serikali inaona ni ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake.

Aidha IGP Sirro alisema kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwanadada huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani

Mbali na hilo  IGP Sirro alisema jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine.

No comments

Powered by Blogger.