KITILA MKUMBO AJIVUA UANACHAMA ACT WAZALENDO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof.
Kitila Mkumbo, amejiuzulu uanachama wa ACT-Wazalendo baada ya kudai
kwamba inamuwia vigumu kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya pande zote
mbili, yaani kwenye chama na serikalini.
Katika barua ambayo Prof. Kitila amethibitisha kwamba ni
ya kwake, ameeleza kwamba kwa kipindi cha miezi 6 ambacho amefanya kazi
serikalini kama mtumishi amekumbwa na mazingira magumu katika chama
hasa pale anaposifia vitu vinavyofanywa na serikali ambayo yeye ni
mtumishi wake.
Prof. Mkumbo amesema ameona ni vigumu kuendelea na
ukatibu mkuu na uanachama wake bila kukwaza viongozi wa chama, hivyo ili
kuepuka mgongano wa wazi wa maslahi amemamua kung’atuka uanachama wake
kuanzia leo Oktoba 9, 2017.
Aidha, Prof. Mkumbo amewashukuru viongozi wote wa chama
kwa ushirikiano wa juu waliomuonyesha tangu walipoanzisha chama hicho
mwaka 2014.
Hapa chini ni barua ya kiongozi huyo kwenda ACT Wazalendo.
No comments