Header Ads

RAIS WA MISRI AMWAGA MAMILIONI KWA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA.

 

Mwishoni mwa juma lililopita ilipigwa michezo mbalimbali ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Urusi mwakani 2018 ambapo timu za taifa za kandanda kutoka katika mataifa mbalimbali zilichuana vikali. 

Moja kati ya pambano ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu ni kati ya timu ya taifa ya Misri dhidi ya Congo Brazaville. Iliilazimu timu ya taifa ya Misri kupata ushindi ili iweze kufuzu moja kwa moja katika fainali za kombe la dunia.

Alikuwa ni mshambuliaji wa klabu ya soka ya Liverpoool ambaye pia nyota wa timu hiyo ya taifa la Misri Mohamed Salah alipachika kimiani magoli mawili dakika ya 64 na dakika ya 95 kwa mkwaju wa penati hiyo ikiwa ni dakika chache zimepita toka Arnold Moutou asawazishe goli kwa Congo yaliyotosha kabisa kuirejesha Misri katika michuano hiyo baada ya kiaka 28.

Baada ya ushindi huo Rais wa taifa la Misri Abdul Fattah Al Sisi  ametoa zawadi ya dola 85,000 kwa kila mchezaji ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 hiyo ni baada ya kukutana na kocha wao raia wa Argentina Hector Cuper.

 

 

No comments

Powered by Blogger.