Header Ads

ORODHAS YA KWANZA YA WANAFUNZI WATAKOPATA MKOPO YAWEKWA HADHARANI NA HESLB


Najua Wanachuo wengi wamekua wakiisubiria hii habari kwa muda na sasa imeongelewa rasmi na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) ambayo leo imetoa orodha ya kwanza ya majina ya Wanafunzi wataopewa mikopo.

Wanafunzi wataopewa mikopo kwenye orodha ya kwanza ni Wanafunzi 10,196 kati ya 30,000 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka mpya wa masomo 2017/2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema zaidi ya shilingi Bilioni 34.6 tayari zimetengwa kwa ajili ya Wanafunzi hao waliopitishwa na kwa mwaka wa masomo wa 2017/2018 Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 108.8 kwa ajili ya Wanafunzi hao wapya 30,000.

Kwa Wanafunzi waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja ambao wana sifa za kupata mkopo amesema watapatiwa mikopo baada ya “kuthibitishwa na vyuo watakavyojiunga kwa ajili ya masomo kwa mwaka huu wa masomo 2017/2018”.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alieleza zaidi kuwa lengo la Ofisi yake ni kuhakikisha majina ya Wanafunzi wote waliofanikiwa kupata mkopo yanatolewa kabla ya vyuo kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu (October 2017).

Vilevile Badru alifafanua zaidi kuwa kwa Wanafunzi waliofaulu mitihani yao na wanaondelea na masomo watatumiwa fedha zao vyuoni kuanzia leo >>> “kiasi cha shilingi Bilioni 318.6 kitatolewa kwa Wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.”
“Tayari Serikali imeshatuma fedha hizo ambapo bodi inahakikisha fedha zinafika vyuoni kabla ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondolea Wanafunzi usumbufu”

Kwenye sentensi nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo wa Bodi hiyo Dkt. Veronica Nyahende amesema kuwa majina ya Wanafunzi wote waliokosea majina yao yatafanyiwa uchambuzi na zoezi hilo likikamilika majina yao yatatolewa.

“Kwa mwaka huu tuliingia kwenye mfumo mpya ambao ni wa mtandao ambapo mwombaji akikosea anaomba upya na kuweka viambatanisho vyote ili kuthibitisha uhalali wake hivyo mwaka huu hatukuwa na utaratibu wa kuwaita waje hapa makao makuu,” alieleza Dkt. Nyahende.

Awamu ya kwanza ya Wanafunzi hao 10,196 waliopata mkopo imepatikana baada ya bodi ya mikopo kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja ambapo sifa kuu za kupata mkopo ni mwombaji awe amepata udahili katika taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na serikali.

No comments

Powered by Blogger.