ORODHA YA NCHI 10 TAJIRI KATIKA BARA LA AFRIKA.
Nchi nyingi duniani zinapambana kuondoka katika janga la umasikini. Katika harakati hizo hapa barani Afrika kuna mataifa ambayo yamepiga hatua kimaendeleo na kuzifanya ziwe juu ya nchi nyingi. Leo nimekusogea mataifa 10 tajiri barani Afrika.
10.Tunisia
Tunisia ina utajiri mkubwa wa mafuta na
gesi na ukiachilia mbali utajiri wa mafuta na gesi, Tunisia ni nchi
ambayo ina vivutio vya utalii vinavyoiingizia pesa.
9.Libya
Libya ni miongoni mwa nchi chache
Afrika yenye uchumi ambao upo juu kutokana na utajiri wa gesi na gypsum
zinazopatikana nchini humo na ni nchi pekee yenye utajiri mkubwa wa
usambazaji wa umeme na uwekezaji wa mafuta.
8. Angola
Angola ni nchi tajiri kwa upande wa mafuta, madini ya almasi ambayo huwa yanasafirishwa kuuzwa nje ya nchi.
7. Botswana
Kiwango cha gharama za maisha kwenye
taifa la Botswana kinalingana na gharama za nchi kama Mexico na Uturuki,
kwa kiasi kikubwa cha uchumi wa nchi hiyo unakuzwa na uchimbaji wa
madini ya Almasi na sifa yake nyingine ni kuwa na idadi ndogo sana ya
watoa rushwa.
6. Gabon
Gabon
utajiri wake ni kutokana na kuwa na madini na mali kwa wingi na
Wafanyabiashara wengi kutoka nchi za kigeni wameweza kuifanya Gabon
kuwa nchi yenye maendeleo barani Afrika kwa kuwekeza biashara zao.
5. Egypt(Misri)
Egypt/Misri ni nchi ambayo ina vivutio
na hiyo inafanya kuwa na watalii wengi ndani ya nchi na nje, inatajwa
kuwa ni moja pia kati ya nchi zilizostaarabika na zimeendelea upande wa
kilimo,maandiko,utawala,dini,vitu vya chuma,pamba na nguo.
4. Equatorial Guinea
Equatorial Guinea ni nchi pekee Afrika
inayotumia lugha ya Kispanyola kama lugha yao rasmi, wanasema moja ya
vitu vinavyokuza uchumi wa nchi hiyo ni mafuta pia ni nchi ya tatu kwa
uzalishaji wa mafuta na vingine kama kilimo, misitu na uvuvi wa samaki
kwa Afrika.
3. South Africa
Uchumi wa Afrika Kusini umeimarika kwa
uuzaji wa madini nje ya nchi kama madini ya dhahabu, almasi na madini
mengine ya chump, hatuwezi kuisahau Afrika Kusini ilipoandaa michuano ya
Kombe la dun mwaka 2010 na kuandaa kwa michuano hiyo kulichangia mapato
ya nchi hiyo kuongezeka na kupata idadi kubwa ya Watalii.
2. Nigeria
Kwa mwaka 2016 IMF waliitaja Nigeria
kama miongoni mwa mataifa yanayotarajiwa kuja kuwa taifa lenye nguvu
kiuchumi barani Afrika baada ya kuipiku Afrika Kusini.
1.Seychelles
Benki ya dunia mwaka 2015 ilitaja Seychelles
kuwa miongoni mwa nchi zinazozoingiza mapato mengi na kukuza uchumi wa
nchi hiyo, inawezekana uwepo wa idadi ndogo ya watu umesaidia nchi hiyo
kuwa na uchumi imara na kufikia kuwa nchi namba moja kwa utajiri Afrika
huku ikitajwa kuwa ina ukosefu wa ajira kwa kiwango cha asilimia moja
pekee.
Imepewa nguvu na mtandao wa nguvu wa millardayo.com. Unaweza kuutembelea sasa.
No comments