MAMBO MUHIMU 9 YA PEKEE USIYOYAJUA KUTOKA KWA MUGABE.
Jina lake huenda ndilo linalotajwa sana katika vyombo vy ahbari kwa sasa. Japokuwa haijulikani ni wapi aliko rais wa sasa wa Zimbabwe, Robert Mugabe, baada ya jeshi kutangaza kuchukua udhibiti Zimbabwe'.
Mugabe, 93, amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu mwaka wa 1980. Alikuwa
Waziri Mkuu hadi 1987 alipochukua usukani kama rais wa nchi hiyo.
Utawala wake wa miaka 37 umeshutumiwa kwa ukandamizaji wa upinzani,
ukiukaji wa sheria za uchaguzi, na kusababisha uchumi wa nchi kuanguka.
shaabanmaulidi.blogspot.com inakusogezea mambo muhimu 9 kutoka kwa Mugabe ambayo huenda ulikuwa huyafahamu.
1) Hapendi kushindwa
Alipokuwa
kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa
tenisi, kulingana na aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki
alikosomea Mugabe. Lakini aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa karata
yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa klabu za Chelsea na Barcelona.
2) 'Kufufuka'
Kuhusu
afya yake, Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema," Nimekufa mara
nyingi-hapo ndipo nimemshinda Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na
akafufuka mara moja," alisema alipotimiza miaka 88.
Ingawa
alilelewa katika familia ya Kikatoliki, alisema alipohojiwa na kituo cha
habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa yeye si
Mkristo anayetumikia dini kwa sana.
3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi
Kwa
muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni
mlezi wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe na nyumba yake ipo
karibu na uga wa michezo wa Harare.
"Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia
inawafanya watu kuwa wema," Bw Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya
Zimbabwe kujinyakulia uhuru. "Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe;
nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana."
4) Mazoezi na vyakula vya kienyeji
Mugabe
anapenda kufanya mazoezi. "Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya
mazoezi ya viungo vya mwili," Bw Mugabe alisema miaka sita iliyopita.
Huwa anaamka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri. Siri nyingine ya
maisha yake marefu ni kuwa anapenda sana 'sadza' - chakula cha kienyeji
kinacholiwa sana Zimbabwe, na ambacho kina virutubisho vingi muhimu.
Vilevile havuti sigara, ingawa hunywa pombe kidogo anapokula chakula cha
jioni.
5) Alipata mtoto akiwa miaka 73
Ana
watoto watatu na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake.
Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga
ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana
na Malaria akiwa na umri wa miaka mitatu Mugabe alipokuwa mfungwa wa
kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.
6) Anampenda Cliff Richard kumliko Bob Marley
Mwanasiasa
wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia
mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya
kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Mugabe hakumtaka mwimbaji Bob
Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa
Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Mwimbaji, Jim Reeves.
7) Mvaaji wa nguo maridadi
Anapenda
sana suti zinazoutosha mwili wake sawasawa na tai zinazofanana na
kitambaa. Huwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake.
8) Anamtazama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake
Bw Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri.
Katika
mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: "Niliwaambia pia kuhusu Kwame
Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza Ghana kupata uhuru; Kwame
aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya
jitihada na kujitolea kwa kila mtu.
9) Ni mtu mwenye shahada nyingi
Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya
kwanza ni kutoka chuo kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini. Alisomea
shahada zake nyingine kupitia mtandao akiwa gerezani.
Shahada hizo ni za: elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Imepewa nguvu na BBC Swahili.
No comments