HATIMAYE MGOMO WA MADAKTARI WAKENYA UMESITISHWA RASMI.
Wakenya sasa wamepata matumaini nmapya
baada ya wauguzi wanaofanya kazi katika hospitali za umma kukubali
kusitisha mgomo wao uliochukua takriban miezi mitano.
Katibu mkuu wa Muungano wa wauguzi {Knun} Seth Panyako aliwaambia wauguzi kurudi kazini mara moja.
''Hatimaye tumesitisha mgomo na tunawataka wanachama wetu kurudi kazini ifikiapo Ijumaa saa kumi na moja jioni'', alisema.
Mwenyekiti
wa magavana nchini Kenya Josphat Nanok amesema kuwa makubaliano hayo na
wauguzi yaliafikiwa baada ya majadiliano makali.
''Tumeafikia
mwafaka na serikali wa marupurupu ya wauguzi pamoja na yale ya nguo za
kazi za wauguzi mbali na marupuru ya kuwa hatarini kulipwa katika
kipindi cha mwaka wa fedha cha 2018-2019'', alisema Nanok.
Kulingana
na makubaliano ,wauguzi wataanza kupokea marupuru ya nguo za kazini za
ksh.15,000 kuanzia mwaka wa kipindi cha fedha cha 2018-2019.
Marupurupu hayo yameongezeka kutoka 10,000 waliokuwa wakipata .
''Marupurupu
hayo pia yataendelea kuongezwa kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo baada
ya kipindi cha bajeti cha 2018-2019'', aliongezea Nanok.
Vilevile
wauguzi hao wataanza kupokea marupurupu ya kuwa hatarini ya kati ya
ksh.20,000 na ksh.25,000 za Kenya kulingana na kundi la kazi alioajiriwa
katika kipindi cha bajeti ijayo.
Nanok amesema kuwa marupurupu hayo yataongezwa hadi ksh.30,000 katika kipindi cha bajeti cha 2020/2021.
Ameongezea
kwamba baraza hilo la magavana limeondoa kesi zote dhidi ya wauguzi hao
mahakamani mbali na kuahidi kwamba mishahara yote italipwa mwishoni mwa
mwaka huu.
No comments