Header Ads

LWANDAMINA KUREJEA DAR LEO, KUJIANDAA NA MBEYA CITY.

Image result for lwandamina wa yanga

Kocha mkuu wa klabu ya soka ya yanga Mzambia George Lwandamina anatarajiwa kurejea nchini leo baada ya kukamilisha mazishi ya mpwa wake nyumbani kwao Zambia.

Licha ya kutokuwepo kwa Lwandamina, klabu ya soka ya Yanga imeendelea na mazoezi chini ya usimamizi wa Noel Mwandila ambaye pia ni Mzambia pamoja na wazawa Shdrack Nsajigwa na Juma Pondamali. Lwandamina hata akifika leo hatoweza kuwahi mazoezi hivyo atajuinga na timu hiyo hapo kesho.
hote cha wiki nzima ya Lwandamina kuwa Zambia, kikosi cha Yanga kimekuwa kikiendelea na mazoezi chini ya makocha Wasaidizi, Mzambia mwingine, Noel Mwandila na wazawa, Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali.   

Jumapili hii Yangainatarajiwa kuwavaa Mbeya City katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu. 

Kwa ujumla baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kirafiki za kimataifa zikiwemo za kufuzu Kombe la Dunia, Ligi Kuu inatarajiwa kurejea wikiendi hii na Ijumaa Singida United wataikaribisha Lipuli ya Iringa Uwanja wa Namfua, wakati Azam FC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC Jumamosi Uwanja wa Saba Saba.
Azam FC wana taji moja tu la Ligi Kuu kwenye kabati lao, walilotwaa mwaka 2013-2014 baada ya kupanda msimu wa 2008-2009.

Mechi nyingine za Jumamosi, Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Stand United n Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Maji Maji na Mbao FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 17, sawa na Mtibwa Sugar, nyuma ya Simba na Azam zenye pointi 19 kila moja.

No comments

Powered by Blogger.